Wednesday, February 20

Kifungua kinywa.....

   Nakuonjesha muonekano wa sandwich ambayo mara kwa mara huwa ninatengeneza asubuhi na kwenda nayo mihangaikoni.
   Uzuri hainichukui muda kutengeneza, yaani utayarishaji hadi mwisho kabisa. La muhimu uwe na sandwich maker ambapo ndo inafanya mpango mzima wa sandwich utokee kama ulivyo kwa picha. Na iwapo hauna hiyo mashine basi waweza kutengeneza na kuila hivyo hivyo bila ya kuweka kwa mashine. Yote ni kheri, ila ladha zinatofautuana.
    Ntakuja kukuonesha step moja hadi ya mwisho ya utengenezaji wake. Na zuri zaidi ni kwamba waweza weka aina yeyote ya ingredients utakayo kutokana na uamuzi wako wa kutaka sandwich ipi.
    Ya leo ni hii, ndani kuna jibini a.k.a cheese na beef sausages


   Huwa natengeneza nyingi kwa ajili ya ndugu na marafiq. Nijuze kama utaipenda na ungependa kuijaribu, anwani yetu ni ileile menutimes@gmail.com
   Kutoka jikoni kwa LJM, tunawatakia siku njema!!

No comments:

Post a Comment