Monday, February 18

Twende Asia kidooooogo

   Wikiendi hii iliyokwisha tulitoka na wanafamilia wanaotuweka mjini, yaani wadhamini wa Menu Time kwa ajili ya chakula cha usiku cha pamoja. Na tukaona ni vyema tusafiri kiladha na kwenda kutembelea bara la Asia. Eneo linaitwa The Great wall Restaurant.
   Kimandhari ni pazuri, eneo la kuegesha magari ni pakubwa tu kwa wale wenye magari yao, urembo ndani umepapendezesha vyema, na uchaguzi wa samani ni mzuri mno. Tukaagiza vyakula tofauti tofauti, cha muhimu ilikua ni mboga ambapo tuliamua kuchukua aina tofauti-tofauti za nyama. Karibu tusafiri sote....
   Muonekano wa chakula chote kwa pamoja pale kilipofika mezani.


 Kulikua na nyama ya ng'ombe ....

Kulikua na nyama ya kuku ....

Kulikua na nyama ya nguruwe....

Kulikua na kamba wa baharini ..... (ugonjwa wa LJM)

 Mboga zote zilisindikizwa na tambi zilizochanganywa na kamba
  
Na wali uliochanganywa na mbogamboga

Ukivipakua vyote katika sahani moja kwa wakati mmoja, sahani yako yaweza kuonekana hivi ambapo kuna milo yote iliyoorodheshwa hapo juu
 
   Kihalali, jumla ya milo yote hiyo pamoja na visindikizio yaani vimiminika vinacost bei ya kawaida sana ambayo familia yeyote yaweza kuafford mara moja moja pale ambapo mna sababu ya kukutana na kufurahi/ kusherekea jambo lolote jema ndani yetu. Sisi tulikua tunasherekea ongezeko la wanafamilia ndani ya familia yetu ya Menu Time.
   Mgahawa huu ni wa kwenda iwapo wataka kupata ladha ya kutoka China, Tunapakubali na kukushauri kwenda kujaribu menu yao.
   Kutoka Oyesterbay ilipo The Great wall restaurant, Dar iliyo Salama, Menu Time inaarifu!!

No comments:

Post a Comment