Monday, March 11

Kifungua Kinywa mwisho wa wiki a.k.a Weekend

   Siku ambazo napata muda kama ilivyo kwa wengi wa kupumzika na kufurahia chakula cha asubuhi yaani kifungua kinywa nikiwa nyumbani ni siku za mwisho wa wiki a.k.a weekend . Aidha iwe ni Jumamosi au Jumapili, napata muda wa kutayarisha vyema kwa ajili ya wanafamilia na pia sote tunapata muda wa kuongea na kujuzana yaliyojiri wiki nzima huku tukipata kifungua kinywa. 
   Jumamosi nilitayarisha haya nilipokwenda kumtembelea mama, yaani nilifanya kuingia jikoni kisha nkajituma ili tufurahie pamoja huku tukisemezana mambo ya mama na wana wake.
   Ushuhuda kwa njia ya picha ni huo hapo ambapo vyote vilikuwa tayari ndani ya muda wa dakika 45 tu. 

   Tukianzia toka juu kwa mzunguko kuelekea kulia, juu, kuna mikate iliyowekwa kwenye moto kidogo a.k.a toasted, kuna viazi vilivyokaangwa na vitunguu baada ya kuchemshwa kidogo na pilipili manga na chumvi, kuna mayai yaliyovurugwa a.k.a scramble eggs yenye nyanya, vitunguu, jibini, maziwa na chumvi, kuna ndizi zilizokaangwa kwenye mafuta kidogo, kuna sausages zilizochemshwa kidogo kisha kukaangwa kwenye mafuta kidogo, na mananasi yaliyowekwa unga wa abdalasini na sukari kisha yakaingizwa kwenye oven kuokwa kwa muda kidogo. Kulikuwa na chai ya maziwa iliyopikwa, ilipikwa na majani ya chai, abdalasini, iliki na sukari kidogo. Baada ya kuiva ikachujwa na kuhifadhiwa ndani ya chupa ya chai ili isipoe.

    Sahani ya LJM ilionekana hivi baada ya kujipakulia tayari kwa kula.
   Ukishamaliza kula vyote hivyo, unaweza kushushia na maji ya matunda au maji safi ya kunywa, itategemea unapendelea nini zaidi. Naamini tutaenjoy kifungua kinywa cha weekend hii.
   Iwapo wataka kujua namna ya kupika chochote ulichopenda hapo juu, tafadhali tujuze kupitia barua pepe zetu. Tunawatakia Wiki njema!!

No comments:

Post a Comment