Wednesday, January 25

Namna ya kupika Ndizi za kusonga na Rost ya Samaki

Mahitaji.
  •  Ndizi Bukoba
  • Samaki (sato)
  • Peanut Butter (karanga za kusaga)
  • Nyanya
  • Kitunguu
  • Pili pili hoho
  • Chumvi
  • Karoti 
Hatua
  • Andaa Samaki wako na mkaange kwenye mafuta
  • Samaki wako akiiva atonekana namna Hii
  • Kaanga vitunguu, karoti, nyanya, hoho, kwa pamoja mpaka viive vizuri kisha weka samaki wako katika mchanganyiko huo, baada ya kuweka samaki wako miminia tui la karanga (peanut butter), subiri mpaka mchanganyiko wako uive vizuri na utaonekana Hivi
  • Menya ndizi zichemshe mpaka ziive ziache na maji kidogo ili ukisonga zisiwe ngumu.
  • Songa ndizi zako mpaka ziwe zichanganyike vema
  • Pakua ndizi zako na uweke Jamvini, mezani tayari kabisa kwa kula. Chakula hiki waweza kukila mchana au jioni ni chakula kitamu sana.
 Karibu sana ukipata ugumu katika kuandaa chakula hiki wasiliana nasi kupitia email yetu menutimes@gmail.com au namba zetu za simu. Menu Time Team

No comments:

Post a Comment