Tuesday, January 31

Mchemsho toka Rock city

   Tulikua kimya kidogo timu ya Menu Time...... msijali tumerejea hewani, ni mambo mbalimbali tu ya kujiboresha zaidi.
    Baada ya mwanatimu mwenzangu kutoka pande za Iringa, mie nikasema nkaangalie Kigoma wanaendeleaje. Nilikatiza Mwanza a.k.a Rock City nikiwa naelekea Mwisho wa reli, Kigoma wikiendi iliyopita. Sasa kwa usafiri wa anga wa kampuni ya Precision, tunasimama kidogo Mwanza, tunabadili usafiri kisha tunasonga mbele kuelekea mwisho wa safari.
    Ni sawa Mwanza yasifika kwa uwepo wa Samaki wa kila aina, si wapo pembeni ya ziwa????? ila haimaanishi nyama nyingine hazipo. Ng'ombe wapo, mbuzi na hata kuku. Nkakatiza pahala (jina kidogo limenitoka ila ntawauliza wenyeji kisha ntawajuza), na hapo nlipata mchemcho wa kuku.

  
Ntakuja kukujuza yaliyojiri Kigoma, Mwisho wa Reli, ambapo baadhi ya wenyeji wangu (Gbee minja na Nesta) wanapaita land of butter and cream.... usiniulize kwa nini.

Kutoka Mwanza a.k.a Rock City LJM naarifu.

No comments:

Post a Comment