Monday, March 11

Yalojiri Safari Larger Nyama choma - Leaders ground!!

   Jumamosi iliyopita kulikua na shangwe pale Kinondoni leaders, ambapo bia ya Safari Larger, kinywaji kinachotengenezwa na TBL walikua na tamasha lao linalojulikana kama Safari larger Nyama choma. 
      SafariLarger Nyama Choma walikua Mbeya wiki iliyopita, ambapo Saigoni bar ndo waliibuka washindi.
   Siku hiyo  wanashindanishwa wataalamu watano kutoka pande kadhaa za Dar iliyo salama, na mshindi wa kuchoma nyama anapatikanika siku hiyo, na walioshindanishwa ni Fyatanga bar waliopo Boko, Uhakika pub ya mtoni Kijichi, Assenga pub ya Buguruni, Titanic bar ya kule Vingunguti na Soccer city bar iliyopo kwa wajanja Sinza.

 Mshindi wa mwaka huu alikua ni Titanic ya Vingunguti. Pongezi sana kwa Titanic kwa kushinda mpambano huu. Itabidi tuje kula nyama na kuongelea ushindi wenu.
   Menu Time toka Leaders inaripoti!! 

No comments:

Post a Comment