Monday, September 10

Ratiba ya Chakula kwa mgonjwa wa kisukari - Siku ya Sita

   Siku ya Sita ndio hii hapa tumekutana nayo, na tunaendelea kuelimishana kuhusiana na menyu anayotakiwa kutengenezewa na kuila Rafiq asumbuliwaye na ugonjwa wa kisukari.
   Tuendelee kukumbuka ya kwamba Rafiq anayesumbuliwa na kisukari hupaswa kula walau mara 5 kwa siku ambapo ni tofauti kidogo na ule mpangilio tuliozoea wa mara tatu kwa siku, yaani asubuhi, mchana na jioni.
    Karibuni...

KIFUNGUA KINYWA:
  • Chai ya Soya au chai ya Maziwa na soya, mkate vipande 2
  
SAA 4 ASUBUHI
  • Juisi freshi au tunda 
 
CHAKULA CHA MCHANA
  • Viazi mviringo, Maharagwe au Njegere 

 

SAA 10 JIONI
  • Kikombe cha Chai ya Soya au tunda

CHAKULA CHA USIKU
  • Ndizi mchemsho na mbogamboga na tunda
 
   Tuseme Asante sana kwa waganga wanaotupatia elimu hii tunayoshare nanyi, na tunaamini kuwa inasaidia wengi wetu. Endelea kutembelea humu, ili upate kujua siku ya mwisho yaani ya saba kuna menu gani ya kuandaa.
   Kama una maoni, maswali na mengineyo usisite kutuandikia kupitia anwani zetu menutimes@gmail.com au menutimetz@gmail.com. Karibuni sana !!

No comments:

Post a Comment