Kumbusho letu ni lilelile ya kwamba, Rafiq anayesumbuliwa na kisukari hupaswa kula walau mara 5 kwa siku ambapo ni tofauti kidogo na ule mpangilio tuliozoea wa mara tatu kwa siku, yaani asubuhi, mchana na jioni.
Haya tumalizie hii siku iliyobakia:
KIFUNGUA KINYWA:
- Chai ya Soya au chai ya Maziwa na soya, mkate vipande 2
SAA 4 ASUBUHI
- Juisi freshi au tunda
CHAKULA CHA MCHANA
- Wali na kuku mchemsho na mbogamboga
SAA 10 JIONI
- Kikombe cha Chai ya Soya au tunda
CHAKULA CHA USIKU
- Viazi mchemsho na mbogamboga na tunda
Sasa tuna ratiba nzima ya Rafiqs wanaosumbuliwa na maradhi ya kisukari. tunaamini vyote vinaeleweka, na iwapo lipo swali, maoni au jambo lolote ungependa kutujuza, tunakukaribisha sana sana.
Shukrani za dhati kwa daktari wa Lugalo kwa kutupatia muongozo huu, ambao utawasaidia wengi kupitia blog yetu.
Siku zilizopita ntaonaje
ReplyDeleteKwenye upande wa Vipengele, chagua Afya njema nao utaona za siku za nyuma. Ukifika mwisho wa ukurasa, chagua habari zilizopita.
ReplyDeleteIwapo hutafanikiwa tujuze anwani ya barua pepe yako tukutumie