Sunday, September 9

Ratiba ya Chakula kwa mgonjwa wa kisukari - Siku ya Tano

   Leo tunaongelea siku ya Tano, na kama ulianza kufuatilia mpangilio huu kwa kuanzia siku ya Jumatatu, basi leo tupo Ijumaa. Tuendelee na menu ambayo Rafiqs wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kisukari wanapashwa kufuatilia katika kutengeneza, kutayarishiwa na hata kuula.
   Tukumbuke kwamba Rafiq anayesumbuliwa na kisukari hupaswa kula walau mara 5 kwa siku ambapo ni tofauti kidogo na ule mpangilio tuliozoea wa mara tatu kwa siku, yaani asubuhi, mchana na jioni.
    Tuendelee mbele sasa!!

KIFUNGUA KINYWA:
  • Chai ya Soya na mkate vipande 2
 
 
SAA 4 ASUBUHI
  • Juisi freshi au tunda
 
CHAKULA CHA MCHANA
  • Ugali wa dona, kuku mchemsho na mbogamboga
 
SAA 10 JIONI
  • Kikombe cha Chai ya Soya au tunda
                            
 
CHAKULA CHA USIKU
  • Wali, mbogamboga na kachumbari ya karoti mbichi na tunda


   Tunazidi kusonga mbele na maelekezo haya. Endelea kutupatia maoni, kutujuza, kuuliza maswali au lolote lingine kama unalo kupitia anwani zetu ambazo ni menutimes@gmail.com na menutimetz@gmail.com.
   Shukrani zetu za dhati ni kwa waganga a.k.a doctors wa Hospitali ya Lugalo iliyopo Dar iliyo Salama kwa kutupatia ufahamu huu ambao tunashare nanyi.

No comments:

Post a Comment