Sunday, September 2

Ratiba ya Chakula kwa mgonjwa wa kisukari - Siku ya Nne

   Mmmmhh siku zinazidi kwenda na leo tupo ya Nne...... ndio tunazidi kujifunza zaidi ni kipi tupike au tule, wale ambao tunasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari !!
   Tunazidi kukumbushana kuwa, Rafiq anayesumbuliwa na kisukari hupaswa kula walau mara 5 kwa siku ambapo ni tofauti kidogo na ule mpangilio tuliozoea wa mara tatu kwa siku, yaani asubuhi, mchana na jioni
     Karibuni:

KIFUNGUA KINYWA:
  • Chai ya Soya na mkate vipande 2 

SAA 4 ASUBUHI
  • Juisi freshi au tunda


CHAKULA CHA MCHANA
  • Viazi mviringo, maharagwe au njegere 

SAA 10 JIONI
  • Kikombe cha Chai ya Soya au tunda  

CHAKULA CHA USIKU
  • Ndizi mchemsho na mbogamboga na tunda 

  Siku zinazidi kuyoyoma nasi tunazidi kukujuza. Tuna imani kuwa vimeeleweka vyema na vinaweza kupikika na kutayarishika.
   Endelea kutupatia maoni, kutujuza, kuuliza maswali au lolote lingine kama unalo kupitia anwani zetu ambazo ni menutimes@gmail.com na menutimetz@gmail.com.
    Tunasema Asante sana kwa Hospitali ya Lugalo iliyopo Dar iliyo Salama kwa kutupatia ufahamu huu ambao tunashare nanyi.

No comments:

Post a Comment