Friday, August 17

Unaikumbuka hii?? Jibini salad

   Unaikumbuka hiii??? kama vile tulishawahi kuiposti kipindi cha nyuma hivi... Yaitwa Jibini salad a.k.a Cheese salad,
   Yaliyomo ndani ni Karoti, Nyanya, Vitunguu, Lettuce, Vinegar, Chumvi kiasi na Jibini ya kukwaruzwa. Unachofanya ni kuvikatakata kwa ukubwa unaoutaka wewe, kisha wavichanganya vyema na kumwagia vinegar juu yake.
   Kisha waandaa kwenye bakuli lako la salad tayari kwa salad yako kuliwa.

   Uzuri wa salad hii ni kwamba waweza kuila muda wowote na kwa chakula chochote. Kwa wale wasiopenda miili minene haswa kina dada, basi wanaweza kufanya ndo mlo wa mchana ila uwepo wa jibini yapasa kupungua kidogo. Pia waweza kula kama kianzio cha menyu kwa wale wenzangu na mimi wanaokula sana kuanzia kianzio, main mlo hadi desert. Pia waweza kula katikati ya milo naongelea saa nne za asubuhi, saa tisa mchana au kum,i na mbili jioni katika kupunguza makali ya njaa.
   Ikipoa toka kwa jokofu, mie binafsi naona kama inaongezeka utamu zaidi. ijaribu kipindi hiki cha skukuu, haswa pale unapolipika pilau lako, kisha ukamiminia hilo salad kwa juu..... utanihadithia utamu wake.
   Toka jikoni kwa MenuTime, LJM naarifu

2 comments:

  1. Tunaipataje hii salad???

    ReplyDelete
  2. Tutafute tunaweza kukufanyia delivery. Namba zetu ni 0784 999 790

    ReplyDelete