Friday, August 17

Ujumbe wa Sikuku zijazo!!

   Sikukuu hiyoooo inakuja, naongelea Idi mosi na Idi pili. Yapaswa tujipongeza kwa kuumaliza mfungo wa Ramadhani kwa Amani na utulivu, nasi wana Menu Time tungependa kutoa shukrani zetu kwa kutualika kupata futari nyumba kadha wa kadha za marafiq.
   MenuTime inapenda kuwashukuru woooote waliotualika, waliotutumia picha zao za futari na za vyakula vingine vya kawaida, waliotusahihisha tulipokosea na hatuna neno zuri zaidi ya Shukrani.


   Tujuzeni mtasherekea vipi, na baada ya sikukuu tuambie mlisherekea vipi. Piga picha mlo ulioutayarisha kwa familia, jamaa, marafiq, majirani na ndugu zako nasi tuta waonesha marafiq wengineo wengi wanaoangalia MenuTime blog waliopo hapa Dar iliyo salama, Tanzania, Afrika na kona mbalimbali za dunia.
   Tunawaomba, sote tusherekee sikukuu hizi kwa amani, usalama, upendo, tuwe makini hasa wale tutakaokwenda sehemu mbalimbali, tuwe na ulinzi wa kutosha kwa wenetu, tusaidie maskini wasiojiweza, wagonjwa na tuwakumbuke katika sala na swala zetu za kila siku na tuombeane maisha mema yanye amani na baraka.
  Shukrani zangu binafsi Lulu John M ni kwa familia ya Mzee Mbura, na mtoto wao ambae ni rafiq yetu  sana kaka Mvumo, familia ya Andrew Mbagga, (asee mama Mbagga aliandaa futari tamu mno), na Rafiqs wengine wote kwa mialiko yenu kwa timu nzima ya Menu Time.
  Tunawatakia Weekend njema na Skukuu njema!!
Wasalaam Menu Time team!!

No comments:

Post a Comment