Monday, August 6

Toka Mtwara - Supu

  Mtwara wametuamsha na picha ya kuanzia siku pamoja na wiki. Kutoka kwa Rafiqs zetu kule, Asubuhi yao wanafungua vinywa kwa style hii.
  Walitugusia na kajiushauri ka bure, ati kama wikiendi ulikua unawaongezea TBL, SBL na wengineo wa masuala hayo kina Johnnie mtembezi n.k, basi huna budi kupata supu kama hii ili uagane nao vyema kabla ya majukumu mbalimbali ya kitaifa.
   Ni supu ya kuku wa kienyeji, chapati pembeni na pilipili na ndimu kama ilivyoa ada ya supu ndio mpango mzima wa kuanza wiki

   Kina Amani, Erick, Da Joan & hubby wa Mtwara mko juu kwenye suala la menyu, asanteni sana kwa kutukumbuka.
   Tujuze waanzaje wiki yako nasi tuwajuze Rafiqs wote wa MenuTime. anwani si unakumbuka???? Karibuni sana!!

No comments:

Post a Comment