Tuesday, August 7

Menyu toka kisiwani Zanzibar

   Rafiq wa Menu Time alikua matembezini huko Zanzibar, kisiwani almaarufu kwa zao la karafuu na pia kwa viungo mbalimbali vya kupika vyakula mbalimbali.
   Wengi mkisikia Zanzibar najua pa kwanza kupakumbuka ni forodhani a.k.a Foro kama wanavyopaita wenyewe wenyeji wa huko, Foro, eneo ambalo ni maarufu sana kwa mauzo ya vyakula mbalimbali vinavyotandazwa juu ya meza, vikiwa vishapikwa mda kidogo, au vingine vyapikwa papo kwa hapo baada ya kutoa oda yako.
   Kutoka Travellers cafe, Junior alipata menyu hii na kutuwasilishia picha ili nasi tuwajuze yapatikana wapi, na nini.
   Menyu yake alokula yaitwa Beef lasagna, mbayo imesindikizwa na kajisalad kwa pembeni.

   Tujuze nawe kupitia menutimes@gmail.com na menutimetz@gmail.com kutoka hapo ulipo ni menyu gani waipata.
   Kutoka visiwani, Ephraim Junior, Rafiq wa menuTime amewakilisha! asante sana Epphy

No comments:

Post a Comment