Thursday, August 9

Biriani toka kwa Rafiqs

   Kutoka kwa marafiq wa MenuTime, jana usiku mmoja wa wanaMenuTime  aliletewa chakula kwa ajili ya kuonja, kukila na kisha kutujuza wengine kwa kutumia picha.
   Menyu iliyoletwa yajulikana kwa jina la biriani ya nyama ya ng'ombe. Si unajua waweza kula biriani ya nyama ya kuku, bata, mbuzi nakadhalika, ila hii ilikua ya nyama ya ng'ombe.
    Karibu kwenye uangalizi wa picha

   Tutajitahidi kupata kujifunza namna ya upishi huu wa biriani, ili tuweze kujuzana sote na pengine kujaribu kuupika.
   Ila kama unajua namna ya kupika basi karibu utufundishe nasi tujue, tutumie mapishi yako kwa email address zetu.
  Kwa niaba ya Timu nzima ya menutime tunawashukuru Rafiqs zetu sana sana.

No comments:

Post a Comment