Nikaomba afanye afanyalo, niweze kuonja menyu hiyo, maana kwa picha ilinitoa mate kidogoooo, hapana sio kidogo niliimezea mate kwa utamu ambao bado sijauonja.
Nilielezwa ni mchanganyiko wa kuku, ndizi, mbogamboga kama karoti, pilipili hoho na mengineyo. Na aliyeipika akaipa jina la Rost chicken in veggies.
Kujua namna ya kupika itanipasa, kupanga nae makutano ili tuchukue mpango mzima kisha kuwahabarisha ili nanyi muweze kujaribisha mapishi haya, ila nakuhakikishia ni tamu sababu nilikubaliwa ombi langu la kuionja na hakika niliikubali.
Jovin wa T.bonaz ndio mpishi wa menyu hiyo, na kutoka MenuTime tunasema Asante sana!!
No comments:
Post a Comment