Jana jioni inaelekea usiku, baada ya futari, Rafiq, dada, pacha, partner na majina mengine kama hayo, alinitumia picha ya menyu anayokula. Cha kwanza nilijawa na mate ya kutosha, cha pili nikataka ntafute helikopta iniwahishe bila kukaribishwa, cha tatu, nkataka oda yangu pekee yaani nimle samaki mzimaaa mwenyewe, na hii yote baada ya kutumiwa picha ya samaki.
Binafsi napenda vyakula vya majini na wadhungu wanaita Sea food. Yaani hawa viumbe kama nimezaliwa nao, au nimekua nao kwa jinsi navyowapenda, au kwasababu Lulu yapatikana baharini?????? Halafu ukutane na Rafiq kawapika wakapikika aseeee..... pata picha, samaki wa kukaanga, halafu kuna kachumbari ya nyanya, vitunguu, pilipili na limau, na mboga za majani vyote vikisindikizwa na ugali lainiiiii...... najua una hamu ya menyu hiyo , ila turudi kwenye topic, pata picha iliyonitoa mate usiku wa jana......
Sitaki kusema sana , toka kwa Halima a.k.a sinigar kasema
Fish used: Sato
Ingredients: Onion, garlic, carrots and green paper with a sprinkle of pilau masala
Baked for 30mins
Nina la kuongeza zaidi ya Shukrani??? Asante Mimah!!!
Kutoka Msasani alipo Mimah, LJM wa MenuTime naarifu.
No comments:
Post a Comment