Tuesday, August 14

Mboga mboga - Spinach

   Kila mmoja wetu ana namna ya upishi wa mboga zake, na haswa mie naguswa mno na wale wanaojua kuikatakata mboga vijipande vidogo vidogo , yaani ukiangalia kwa harakaharaka waweza dhani ni mashine imetumika.
   Nina mamamdogo ambae aliniambia, mwanangu ntafutie kisu kikali, nipatie hizo spinach halafu nitazishughulikia. Nami nikafanya hivyo na hii picha hapo chini inaonesha wakati wa ukataji, ilibidi niibie picha ili tuweze kuona

   Upishi wake Spinach hii ni kwamba, unaweka mafuta ya kupikia kwenye sufuria, chumvi kiasi, kisha wakaanga vitunguu maji vyako, utaongeza vipande vya karoti baada ya vitunguu kuiva vyema, baada ya kuiva vyema mchanganyiko wa vitunguu na karoti, unaongezea spinach zako zilizooshwa vyema kabla ya kukatwakatwa, nazo wazikaanga kwa muda kidogo tu, na mpango mzima unatokea kama hapo chini.


   Kutoka jikoni kwa mama Menutime, shukrani sana kwa mama mdogo.

No comments:

Post a Comment