Tumerejea tena kwa waitaliano au niseme restaurant inayopika menyu za kiitaliano. Nia na madhumuni ya kurejea huku ni kujua menyu nyingine ambazo wanaandaa wapishi wa restaurant hii, kwasababu ubora wanaoutumia katika uandaaji wao ni wa hali ya juu. Tusifanye kuongea saaana tuache picha zikuhadithie zaidi.
Hii inaitwa
Lagliata di manzo ai ferri, mlo huu umetengenezwa na viazi vilivyopondwa a.k.a
mashed potatoes na nyama ya ng'ombe, na kasalad ka kusindikizia mpango mzima.
Ya pili yaitwa
Saltimbocca alla furlana, kihaki kabisa, nilivyokula nyama hii nilihisi inayeyuka mdomoni maana ni laini balaa. Ushauri wa bure: kama una mtoto wa mizi 8 -12 na anapenda nyama au ungependa ale nyama na vijimeno vyake kadhaa nahisi kama atamaliza sahani hiyo mwenyewe, maana yasindikizwa na viazi vya kupondwa a.k.a
mash potatoes, hivyo hana kazi sana ya kutafuna mlo wake.
Bado najifunza kutamka hizi menyu ila naamini nimepatia kuziandika (nakubali kusahihishwa). Tutarejea tena kwa mara ya mwisho kuwaonesha tena upikaji wa menyu za
Trattoria Pizzeria iliyopo Oysterbat Dar iliyo salama, sehemu tulivu ya kupata menyu mbalimbali za uhakika na ubora uliopita viwango.
Tuwatakieni wiki njema katika kutimiza majukumu yenu ya kuendeleza Taifa.
Kutoka Oysterbay, restaurant iliyosheheni vyakula vya kiitaliano, LJM wa MT naarifu!
No comments:
Post a Comment