Kuna baadhi ya Rafiqs zetu kula matunda ni issue flani hivi, aidha hawaoni umuhimu wake, au hawajui wapi wanunue (sababu hii siikubali sana maana siku hizi kila kona, matunda yanauzwa... wewe tu na pesa yako na chaguo lako), wengine ati daktari hajawaambia.... wengine hawapendi, yaani tukianza kuongelea sababu za Rafiqs kutokula matunda tutapata nyingi sana kuliko tunavyofikiria.
Sasa mimi ntakuelezea namna chache tu za kula tunda na kuweza kulifurahia na hapo hapo mwili wako ukapata rutuba na virutubisho kadhaa vipatikanavyo kwenye matunda. Ndio moja ya kazi yetu Menu Time ni kufundisha pia.
Waweza kula tunda kama kikorombwezo cha mlo wako (kama vile nawaona wanaokula pilau na ndizi mbivu tena kisukari), waweza changanya matunda kadhaa na kuyala pamoja a.k.a fruit salad, waweza yasaga matunda na kutengeneza kimiminika a.k.a juice na kuinywa.
Hii ni fruit salad.
Hapo juuu kuna mchanganyiko wa matunda kadhaa, naongelea ndizi, tikiti maji, maembe, papai na machungwa na maji ya machungwa. Ukishachanganya matunda haya hauhitaji kuongeza utamu mwingine wowote maana yenyewe yana utamu wake wa kipekee na wa kutosha tu.
Utundu mwingine waweza kufanya ni kuongeza jipande la icecream kwa juu na kuiacha iyeyuke kidogo, kisha pata kula fruit salad yako kwa raha, na joto la Dar iliyo salama
Haigharimu sana, ila huongeza virutubisho mwilini na pia ngozi hung'ara vyema.
No comments:
Post a Comment