Sunday, June 3

Samaki Sato

  Aina hii ya samaki hupatikana ziwa Viktoria pekee, ni samaki watamu ukiwala katika mapishi ya aina zote, tunaongelea wa kukaangwa, wa kuchemshwa, na hata wa kuungwa na mchuzi pia. Hapa Timu ya Menu Time imeletewa zawadi kutoka Mwanza, na Kama ilivo ada Timu yetu imeamua kukuonesha namna mbalimbali za kumpika ama kumtayarisha samaki huyu.

Uzuri aliletwa tayari ashakaangwa, kama aonekanavyo hapo chini

 Sasa waweza kumuandaa kwa kumpasha moto, kisha katakat kachumbari yako na kumla samaki huyu kwa kachumbari.

 Pia waweza kumuandaa ukamla chukuchuku, mchukue samaki wako, muoshe, kisha muweke kwenye sufuria weka na maji kidogo na pili pili, mchemshe mpaka maji yawe rangi ya njano hivi.
  Baada ya hapo pakua kwenye sahani au Bakuli tayari kwa kula.
 Ni samaki mtamu sana, pia wakati wapata kula samaki wako, waweza kujisindikizia na ugali, wali, chapati, yaani ni wewe tu na kile upendacho. Ukija kwenye kishushio ama tuseme kimiminika, waweza tumia juisi, chai, maji, soda na kdhalika..... je wewe wapenda nini? Tafuta samaki wa Sato kisha jaribu aina hizo za upishi tulizokuwekea hapo juu, kisha tutumie picha ya mlo wako ulifananaje kupitia menutimes@gmail.com . Karibu Menu Time.

No comments:

Post a Comment