Tunaongelea tunda la Tikiti maji, na ukitaka kipande kimoja kama hiyo piccha hapo chini itakugharimu shilingi za kitanzania 200 tu.
Thursday, May 31
Tunda la Tikitimaji.
Jioni ya leo, mida ya saa moja moja hivi mitaa ya Buguruni Sheli, Dah!!! yaani kuna mkusanyiko wa watu wengi na shughuli za kila aina hufanyika pale. Jicho la Menu Time lilivutika saana na hiki kitu.
Tunaongelea tunda la Tikiti maji, na ukitaka kipande kimoja kama hiyo piccha hapo chini itakugharimu shilingi za kitanzania 200 tu.
Aina mbalimbali za vipande vimetayarishwa kulingana na mfuko wako, vipande vyenye ukubwa huo hapo chini utajipatia kwa shilingi 500 tu.
Mwisho wa siku mdau wa Menu Time akajipendelea na kipande cha tikitimaji.
Kwa wale marafiq ambao hawana mapenzi ya kunywa maji, au wanapitiwa na zoezi hilo la kunywa maji, ilihali sote tunajua umuhimu wa maji mwilini, wanaweza kuwa wanakula tunda hili mara kwa mara maana lina maji mengi. Hii itasaidia kupunguza upungufu wa maji mwilini mwako. Jitahidi upate la kwako leo.
Tunaongelea tunda la Tikiti maji, na ukitaka kipande kimoja kama hiyo piccha hapo chini itakugharimu shilingi za kitanzania 200 tu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment