Moja ya zao linalolimwa Iringa ni chai. Nilikatiza Mufindi na kwa mbali nikayaona mashamba ya chai. Kuna baridi mno na ukungu wa hali ya juu. Lakini ndio hali ya hewa ambayo chai hunawiri na kukua vyema. Nikasema nisiondoke hivihivi, walau tupate picha japo ya mbali nasi tuione Mufindi ilivyo.
Karibuni
Nilikua na kamera ndogo ambayo ilikua ndo mwisho kuvuta picha, na kwasababu ya baridi hili, nilihofia kushuka.... ila naamini umepata picha ya Mufindi pakoje... wakisema pana baridi wanamaanisha ni baridi kama hivi!!
Bado naarifu toka Iringa, ni LJM
No comments:
Post a Comment