Saturday, April 28

Iringa - Neema craft Workshop

Iringa ni mkoa wenye historia nyingi sana, kulikua na chief Mkwawa, kuna mbuga za wanyama yaitwa Ruaha National Park, ila mimi kivutio nlichopenda, au niseme historia niliyonayo na mkoa huu ni mlo nilioupata Neema Crafts Workshop.
Humo ndani unakutana na bidhaa nzuri tu zilizotengenezwa na wanachama wake ambao wana ulemavu mbalimbali, kuna amabo hawawezi kusikia, au kutembea vyema, ila ni wachapa kazi na wana akili na maarifa mno!!
Restaurant yao wanapika wenyewe na kuhudumia pia. Ni sehemu ambayo hupaswi kuacha kwenda kama utapita Iringa.
Hiyo yaitwa Beef Lasagna. Kila nkiingia Iringa, kituo cha kwanza ni Neema Craft Workshop na menyu ya kwanza ndio hiyoo, nkishushia na juice bariiiidi .


Salad kwa pembeni na parachichi vikisindikiza mpango mzima wa lasagna.
Kutoka Iringa, LJM wa MenuTime naarifu.

No comments:

Post a Comment