Wednesday, March 14

Utengenezaji wa Sandwich ya mayai

   Mlo wa sandwich waweza liwa muda wowote na kinywaji chochote. Ni rahisi kutengeneza na kula pia. Wengi ambao hupenda kubeba kifungua kinywa sandwich ni mojawapo ya menyu inabebwa saaaana nikiwemo mimi.
   Nakuonesha natengenezaje sandwich ya harakaharaka kwa kutumia mayai na mikate. Karibuni

Mahitaji:
  • Mikate vipande viwili
  • Mayai mawili
  • Peanut butter
  • Nola sandwich spread (Inapatikana Shoprite Supermarket)
  • Chumvi kiasi
  • Maziwa vijiko vikubwa vitano
  • Jibini kiasi ya kukwaruza (kama utapenda)

    Hatua:
  • Koroga mayai, maziwa na chumvi kiasi
  • Weka kikaangio kwenye jiko, ongeza mafuta. Yakishapata moto weka mchanganyiko wa mayai yako na kaanga yaive, ongeza jibini kisha geuza upande wa pili nao uive vyema
  • Chukua kipande cha mkate na upake peanut butter na kipande kingine paka Sandwich spread

  • Weka yai lako katikati ya vipande vya mikate, kata kipembezoni (ili iwe rahisi kubeba wakati wa kula) na sandwich yako ipo tayari kuliwa, waweza ongezea na soseji moja hivi
  • Sandwich hii yaweza kuliwa na kinywaji aina ya chai ya rangi, ya maziwa, kahawa, maziwa fresh, juice, soda yaani chaguo ni lako.
 Kutoka jikoni la MenuTime, hilo ndo pishi la leo. Dakika 10 tu umepata chakula chako au waweza hata kuifanya iwe lunch box ya mtoto wako/ ya kwako au mwenza wako.

No comments:

Post a Comment