Tuesday, March 13

Nyama ya Mbuzi ya Ilala

   Kuna bar moja ipo mitaa ya Ilala, ni maarufu sana kwa uchomaji wa nyama, haswa ya mbuzi. Naseme hivi kwasababu mimi na rafiqs zangu huwa tunakwenda kila Alhamisi kupata mbuzi choma na ugali.
   Kusindikiza mlo wako wanakupa na mboga za majani, bamia kidogo na nyanya chungu. Pilipili na chumvi ni viungo muhimu kuwepo. Mida ya saa 6 mchana unakuta mbuzi yupo tayari kwa kuliwa.
   Sehemu yaitwa Miami Beach bar.

Hili ndilo jiko linalotendea haki nyama ya mbuzi

Hapa ipo tayari kwa kuliwa

Ndimu na chumvi kwa kusindikizia menyu hii

Ukiwa mitaa ya Ilala pita hapo nawe uionje

Kutoka Ilala, LJM naarifu

No comments:

Post a Comment