Monday, March 12

Safari Nyama Choma competition - Leaders

   Bado nipo maeneo ya Leaders naendelea kukujuza yale tuliyokutana nayo.

   Watu wakiwa wanongelea nyama choma competition wanamaanisha katika style zote za upikaji na upakuaji. Kutoka banda la Kisuma ambao ni walikua washindi kwa mara nyingine tena, maana wamekua washindi katika miaka 3 iliyopita na mwaka huu wameshinda. Sasa katika kuonesha ujuzi wao, walikuwa na ndafu pale

   Kuku nao walikua na sehemu yao katika mashindano haya, kuna mbuzi na ng'ombe pia katika jiko hili. Hawa ni Titanic bar

   Usije ukadhani ni mtori, rangi yake inavutia mno, ladha yake nayo ni nzuri na tamu. Hii pilipili ilikutwa banda la hao washindi yaani Kisuma na ukinunua nyama pale wapata na pilipili hii ya kukusindikizia. Asee ni tamu mno, mpishi yuko juu

    Kuku kwa karibu zaidi

   Mbuzi kwa kuiona tu, unaijua, haiitaji uwe mzoefu saaana, Kipande tayari kwa kukatwakatwa na kuuzwa. Tuikutana nayo katika banda la Fyatanga


Nyama nyama nyama

Kuna walioamua kuweka matunda na sio kwamba mpaka Daktari aseme, ni katika hali tu ya kuujenga mwili.

Matukio zaidi

 Vya kusindikizia nyama vilikuwepo, naongelea ndizi na chipsi.

Wachagga walirejeshwa nyumbani katika style hii ya ndizi

No comments:

Post a Comment