Thursday, March 15

The Safari Lager Nyama Choma Festival yajaaaa - Dar iliyo salama

   Siku itakua ni Jumamosi tulivu ya tarehe 17 mwezi huu wa Machi, Eneo ni pale viwanja vya Posta, almaarufu eneo la Sayansi, zamani kidogo Airtel walikua na ofisi zao pale na sasa wapo TTCL. Panaitwa Kijitonyama Postal Grounds.
   Muda kuanzia njaa inaposhika namaanisha saa 6 za mchana mpaka kwenye 4 za usiku. Yaani Rafiqs mna masaa 10 ya kula nyama, kula nyama na kula nyama. Kutakua na nyama za kila aina naongelea ya kuku, samaki, ng'ombe, mbuzi na nyingine utakutana nazo pale. Wote mnakaribishwa kwa kiingilio cha 5,000/= tu Mlangoni
   The Safari Lager Nyama Choma Festival ndo hiyoooo mlangoni mwako. Siyo ya kukosa Rafiqs!!!

      Kama kawa MenuTime Team tutakuwepo Kijitonyama Postal Grounds kuwakilisha na tutarejea hapa kwenye blog na kuwajuza yatakayojiri Jumamosi hii tarehe 17/3/2012 kwenye The Safari Lager Nyama Choma Festival.

No comments:

Post a Comment