Friday, March 16

Matunda

   Kikawaida tumezoea kula matunda baada ya mlo, na wengine mpaka tukitoka kutibiwa na kushauriwa kula matunda, ndo tunawajibika kula matunda.
   Matunda ni chakula muhimu sana kwenye  maisha yetu na haswa katika kujenga miili yetu. Uzuri wa kula matunda waweza kula katika muda wowote, yaani asubuhi waweza kula kipande cha tunda lolote, mchana au hata kati ya asubuhi na mchana naongelea saa 4, kuna baada ya mchana yaani saa9, au 12 jioni na hata katika mlo wa usiku.
 
   
    Pia waweza kutengeneza juisi ya matunda na kuinywa badala ya kulila tunda lenyewe. waweza changanya tunda na icecream au mtindi na kutengeneza ladha tofauti na kuila kama desert, yaani ni wewe na ubunifu wako unataka uyale vipi hayo matunda yako.
   Tutarejea kuwajuza zaidi kuhusiana na tunda moja baada ya jingine na jinsi gani yanasaidia kuboresha miili yetu. Hii tutaanza wiki inayokuja

No comments:

Post a Comment