Friday, February 3

Supu ya Kitaani

   Kama vile MenuTime tumeamua kuongelea supu zaidi. Lakini kuna sifa mbalimbali za supu tungependa mzifahamu.
  • Supu huliwa kama kifungua kinywa,
  • Supu ni nzuri na hutumika kukata/ kuondoa mning'inio a.k.a hangover,
  • Supu nzuri kwa wasiopenda kula ni rahisi kuinywa kama mlo mbadala,
  • Supu, kwa wanaofanya mazoezi ya kupunguza kula a.k.a diet ni mlo mzuri (ila isiwe na mafuta saana),
  • Halafu ni rahisi mno kuitengeneza supu, kwa namna uipendayo. haitumii mda sana kama kupika mlo kamili,
  • Kwenye shughuli mbalimbali na hata katika milo ya mchana na usiku supu hutumika kama kifungulio mlo a.k.a starter.
  • ........ na kadhalika.
Mitaa ya Chang'ombe almaarufu kama Maduka mawili nilikutana na supu hizi mbili.

Kuna hii ya mbuzi unashushia na kachapati kidogo,

Halafu kuna ya kuku wa kienyeji na wa kisasa. Hii niwa kienyeji, yaonekana laini mnno

      Ukifika Chang'ombe uliza wapi Maduka mawili yapo, nenda kajipatie supu yako.
Tujuze wewe wapendelea supu gani na waipata maeneo gani, kupitia menutimes@gmail.com tuweze kwenda kuijaribu na kuwahabarisha wenzetu.
      Tunawatakia Weekend Njema

No comments:

Post a Comment