Thursday, February 2

Mwanza Mwanza

    Bado nipo na wana Rock city, na menyu zao..... kama vile nimewapendea wanywa supu zaidi au???. Basi naendelea kuwajuza menyu zao wenzetu wa Mwanza. Nlichopenda zaidi ni supu ya samaki na sio mchemsho wa samaki. Mie kama nimezoea kukutana na mchemsho wa samaki ambae anakuwa mzima, unakutana na ndizi na viazi kidogo, na mambo mengine mbalimbali.
   Sasa ukitua kiwanja cha ndege cha Mwanza, ukitoka pale nje, ukiangalia mbele yako kuna baa moja hivi. Pale ndo utakutana na mambo haya.....
   Chagua wataka kipande cha kati???

   Au wataka mkia?? kuna kichwa pia nalo ni chaguo vilevile. Pilipili, ndimu na chumvi wasindikizaji tu hawa.

      Kama we si mkazi wa Mwanza, na katika matembezi yako umepania kula samaki, ushauri wetu ni anzia hapo kama umetua na ndege... kunywa supu, safisha tumbo na weka tayari kwa menyu zingine zinazofuata. Waweza kunywa wakati unarejea ulipotoka, ila uwahi kabla ya muda wa kucheck in la wawezwa achwa na ndege kwa utamu. Karibuni Mwanza!!!

  Kutoka Rock City kama wapendavyo kupaita, jina lake halisi Mwanza, LJM naarifu.

No comments:

Post a Comment