Wednesday, February 22

Forodhani - Zanzibar

   Forodhani a.k.a Foro ni eneo linalojulikana kwa uuzwaji wa vyakula mbalimbali. Wakazi, wenyeji na wageni hutembelea hapo kujipatia vyakula na juisi mbalimbali haswa za miwa. Kuna vyakula mbalimbali kuanzia nyama za ng'ombe, samaki aina kadhaa, chapati nzito, za maji, za kihindi, chipsi, ndizi n.k yaani wewe, hamu yako, pesa yako na chaguo lako tu.
  
  Karibu upate kujione vyakula vinavyopatikanika Forodhani almaarufu Foro:

Kuna kila aina ya samaki katika mapishi mbalimbali...

Pia kuna mishkaki ya kuku, samaki, yenye pilipili, ndizi...

 Pia mishaki ya nyama nyekundu ipo, ya maini ipo .....

Hapa ndio forodhani bwana, sehemu ambayo lazima uipitie, na kujaribu vyakula vyake ukienda kisiwa cha Zanzibar.

No comments:

Post a Comment