Tuesday, November 1

Bado niko na Wahehe - Iringa

Nilivyoondoka Iringa, nilipata lawama kwamba sikuonesha picha halisi za nyama tuliyoenda kuisabahi pande zile za Igingilanyi.

Nikasema mie sio mchoyo, hivyo basi karibu uone yaliyojiri kule Iringa mwezi jana.....

 Hapa nyama baada ya kuchaguliwa inachomwa tayari kwa kuliwa:

Imeletwa mezani, tayari kwa kushambuliwa; uzuri wa namna ya kula hii nyama ni kwamba yule aliyeichoma anaikatakata na kuwapa vipande walaji huku akiwazunguka duara mpaka nyama yote inaisha

Pia ukipenda ikatwe katwe jikoni na uletewe ikiwa tayari, wanafanya hivyo, Ukitaka kachumbari, pesa yako tu unaamua ya shilingi ngapi. Sasa huu mlo ni ule unaotayarishwa hukohuko jikoni

No comments:

Post a Comment