Thursday, October 6

Moshi Leopard Hotel

Baada ya ile Pizza niliyopata kuionja pale Leopard Hotel, kabla ya kerejea Dar, nikaomba wanitengenezee anything Italian, kuna filamu yenye asili ya uitaliano nilikua naangalia, halafu mmoja wa waigizaji akaelekea restaurant akanunua wrap up pizza au jina kama hilo. Yaani nilishindwa kuendelea kuangalia..... nikawatafuta Rafiqs wanihabarishe, kwa Moshi wapi ntapata hii menyu??? Mac Temba akaniambia tafuta Leopard ukidhi haja yako.
Nikajongea, nikaongea na chef pale, tukaelewana na hii ndo alichotoa baada ya kujaribu kumuelezea bila ya kuangalia menyu.

Usijichoshe kujiuliza kuna nini ndani, niliikata kuchungulia je yaliyomo yamo??? na hivi ndivyo nilivyokuta...... Karibu.

Asante sana Priscus na wahudumu wote wa Leopard Hotel, bila kumsahau fundi wangu, ndioooo naongelea mpishi mwenyewe, maana nisingelala usiku ule.Asanteni Moshi!!

No comments:

Post a Comment