Thursday, October 6

Menyu ya Mwisho ya Moshi

Kabla ya kuondoka, nikasema wacha niangalia Samaki wanapikwaje huku Moshi??? Wakaniambia wanapika, wewe tu useme wataka kula na nini..... na wao wanakutayarisha kwa vile utakavyochagua.

Fish fillet, kamboga kwa mbaaali na mash potatoes yaani vile vilivyopondwa.

Kilichokwenda Wrong: Mteja anapoagiza mash potatoes, naamini anataka mash potatoes, na sio viazi vilivyokatwa vipande vidogovidogo. Na kawaida huwa vinapondwa vikichanganywa na maziwa kidogo, butter na la msingi vinapondwa haswaa mpaka vinalainika. Haitakikaniki kukutana na mabongemabonge wakati unakula. na kwa menyu hii Impala hotel ndipo walipoenda wrong kwa kweli. Next time i hope wataponda vyema kiwe ka cha mtoto wa  miezi 5.

No comments:

Post a Comment