Friday, September 2

Menyu ya Mgahawani

Siku mbili tatu hapo nyuma kuna Rafiq yangu aliniambia niambatane nae nikale msosi wa aina mbalimbali kwa mara moja.....Upo?? yaani nipate kuonja aina mbalimbali ndani ya sahani moja.... kama utani vile eee? ila ni kweli.
Eneo ambalo menyu hii inapatikana ni pale Savannah lounge iliyopo Quality center, Nyerere Road. 


Ukifika we ulizia " Mixed grill" halafu uonje au ule kabisaaaaaa, huku unashushia na kinywaji upendacho. Mie maji yasiyo baridi yalinitosha kushushia. Ila wanyewe wana kila aina ya vinywaji, wewe tu na chaguo lako.
Mixed grill ina maini, kuku, nyama ya ng'ombe, sausages yaani full nyama, afu vyote vimewekwa kwenye jani lenye ladha, pembeni kuna aidha wali au chips au kingine upendacho.......

No comments:

Post a Comment