Monday, September 5

Menyu ya hotelini - Tilapia

Ukifika Mwanza a.k.a Rock city, lazma upige picha na yale mawe, pili ile sanamu ya Samaki pale Round-about usisahau nayo, afu upate kula samaki wa aina na mapishi mbalimbali.
Hii inapatikana Hotel Tilapia,

Jina la menyu hii ni " Fish fillet meuniere". Binafsi nimeipenda sababu ya inawekwa ladha ya ndimundimu hivyo hauikinai, haswa kwa wale wasiopenda sana samaki. Vimbogamboga hivyo navyo vimechemshwa kidogo na chumvi kwa mbaaaaaali.
Agiza na chochote cha pembeni iwe wali, viazi vya kuponda au kukaanga ni wewe tu na chaguo lako. Usisahau kishushia menyu !!! Karibu

No comments:

Post a Comment