Wednesday, August 10

Macaroni yenye limau

Mara kwa mara nikiangalia vipindi vya mapishi, wenzetu mara nyingi sana hutumia jibini a.k.a cheese. Unakuta add a bit of cheese halafu unamwaga cheese ya kutosha, sasa mie huwa najiuliza kama hiyo ndo kidogo je wakisema nyingi itakuaje?

Nimegundua kitu kimoja, kununua jibini kiswa ukaikwaruza mwenyewe kwa matumizi yako ni rahisi kidogo ukilinganisha na kununua jibini iliyokwaruzwa tayari.

Karibu kwenye mapishi ya macaroni na mchuzi wa limau a.k.a macaroni with lemon juice.

Mahitaji:
  • Pakiti moja ya macaroni
  • Maji safi
  • Pilipili manga kiasi a.k.a black pepper
  • Chumvi kiasi
  • Abdalasini kiasi a.k.a cinammon
  • Jibini iliyokwaruzwa ya kutosha a.k.a cheese
  • Limau kubwa moja - ioshe vyema
Hatua:
  • Tayarisha maji kwenye sufuria, ongeza chumvi kiasi, pilipili manga na abdalasini, funika mpaka yachemke kabisa, yatakua yanatoa harufu nzuri sana ya viungo hivyo
  • Weka macaroni yako ndani ya maji yaliyochemka kisha yaache yaive. Mara nyingi kwenye pakiti wanaandika dk za kuchemsha macaroni, ila mie naona ni vyema uyaonje na kuhakikisha yamechemka vyema, usije walisha familia na rafiqs chakula ambacho hakijaiva
  • Epua macaroni yaliyoiva kisha uyachuje maji yabaki makavu
  • Chukua chombo cha kuokea kwenye oven, kisha yaweke macaroni yako
  • Chukua limau moja na kwaruza maganda yake na kuyachanganya na macaroni
  • Kamua hiyo limau na ile juisi yake ichanganye kwenye macaroni, kisha koroga yema kuhakikisha juisi na maganda yaliyokwaruzwa yamechanganyika vyema na macaroni
  • Chukua jibini yako uliyoikwaruza na kuitandaza juu ya macaroni yako yenye mchuzi wa limau
  • Weka jibini ya kutosha kisha ingiza chombo chako kwenye oven kwa kuivisha kwa dk kama 5 kuruhusu ile jibini iyeyuke na kuchanganyika vyema na macaroni yako
  • Epua mlo wako tayari kwa kuliwa.
Mlo wangu mie ulitokea hivi:

Waweza kushushia na kinywaji cha aina yeyote kile, wewe tu na mapenzi na chaguo lako.

No comments:

Post a Comment