Thursday, August 11

Chipsi, mayai, salad vyote vina jibini kidogo

Ni rahisi sana kupika chakula kile upendacho na kuweka viungo uvitakavyo katika ujazo uutakao, ndicho haswaa kinachonifanya nipende kupika mwenyewe kwa ajili yangu, familia na marafiki zangu.
Ukitaka kujua nilipikaje futilia hapo chini na ukiwa na swali zaidi, tafadhali niulize nitakuhadithia ila Menyu ya leo ndio hii.... Karibu:

Chips hizi nilizikaanga zikiwa nimeziweka chumvi, kisha zilivyotoka jikoni nikanyunyuzia jibini iliyokwaruzwa, sausages nilizikaanga tu na mafuta ya olive kidogo, salad ni mchanganyiko wa nyanya, kitunguu maji, karoti iliyokwaruzwa, lectuce iliyokatwakatwa pamoja na jibini kidogo iliyokwaruzwa, na mayai yalikorogwa huku yakichanganywa na maziwa, cheese iliyokwaruzwa kidogo, chumvi na kukaangwa na mafuta kidogo ya olive na kitunguu swaumu. 

No comments:

Post a Comment