Thursday, July 21

Bukoba

Nyama choma hupatikana kila mkoa naamini, Bukoba a.k.a BK nao hawako nyuma kwenye uchomaji wa nyama. Menyu ya tano iliyokutwa BK ni ya uchomaji. Jioni flani watu wakiwa wamejipumzisha baada ya kazi ndefu na nzito za ujenzi wa Taifa, basi huwa hujisogeza pembezoni mwa ziwa na huagiza menyu kama hii.

Hapo kuna ndizi mzuzu, nundu na ulimi vyote vimechomwa. Pilipili na chumvi kidogo kuongeza ladha, ndimu kama utapenda pia ndo kilichokutwa na Camera yetu.

No comments:

Post a Comment