Thursday, July 21

Bukoba

Bukoba raha yake Samaki, huku wapata samaki kwa kupikwa kwa aina tofautitofauti. Kuna wa kuchoma, wa kukaanga, wa mchuzi hata rosti, wa foil, mchemsho yaani wewe vile utakavyo.
Menyu ya nne toka Bukoba ni mapishi ya samaki wa foil. Ushahidi ndo huu:

Huyu anapikwa kwa moto kidogo akiwa ameviringishwa ndani ya foil na viungo kadhaa vya kumuongezea utamu. Halafu anaandaliwa wamotomoto hivyohivyo... hakika usipoangalia vyema waweza ungua vidole maana kusubiri apoe sidhani kama utakua na subira hiyo.

No comments:

Post a Comment