Friday, May 31

Lunch ya Furahiii day hii.

   Ijumaa ya leo, ambapo ndio wikiendi inapoanza, tunapitisha mchana kwa menu hii ya pale pale Filigisini. 
    Ni chipsi na firigisi mix na maini. Karibu

        Kwa karibu kabisa !!!

       Ndo mlo wetu huu!!
    Hope mmekua na mchana mwema kwenu kama ilivyo kwetu. Karibu kushare nasi Rafiq.

Thursday, May 30

Firigisi na ndizi ndo menu ya mchana

   Mchana wa leo tumerudi pale pale Firigisini, maana mlo wa jana ulituvutia. Ila leo tumebadilisha badala ya ugali tumechukua ndizi.

    Ilikua tamu sana na huo ndio mlo wetu kwa siku ya leo, mchana wa leo
   Karibu kushare nasi mlo wako wa leo

Wednesday, May 29

Ugali mchana wa leo

Mchana wa leo Jumatano hii, ulitukuta pande za Kinondoni kwenye sehmu ijulikanayo kama Filigisini. Hapo ni maarufu kwa mapiko ya firigisi, na hapo chini ni moja ya mmsosi uliopatikana hapo. Ni firigisi rosti yenye vitunguu vingi na ugali.

    Kwa karibu zaidi.
   Kesho tutakujuza nini cha mchana

Tuesday, May 28

Cha mchana Jumanne hii ni .......

   Bado tuko pande zilezile za Samaki Samaki ya mjini posta. Dar iliyo salama ukisema mjini shurti utaje na posta kidogo ndo tuende sawa. Sasa basi kama ilivyo kwa wengi ukienda sehemu kula unakua na kampani aidha awe ndugu, rafiq, mfanyakazi mwenzio au hata adui yaani mnaenda kuzinguana sehemu ya kula ili kumalize tofauti zenu.
   Sahani ya kampani tuliyokua nayo ni hii hapa, yaani yeye alipenda zaidi mlo huu kama menu yake ya mchana hapa Samaki samaki

  Kama kawa viazi vyao vina saizi tofauti kidogo, ambapo Rafq aliagiza na ngisi a.k.a calamari

  Vikorombezo kwa pembeni, wakina pilipili, ndimu, mayonnaise na tomato sauce waliambatanishwa kuongeza ladha kwa Rafiq. Mboga za majani nazo pia huwekwa kwa mbali katika  mlo huu ili kuhakikisha unapata mlo proper

   Karibu kushare nasi menu uipatayo mida ya mchana ili nasi tushee na wao!! barua pepe ni ileile menutimes@gmail.com

Monday, May 27

Chakula cha mchana

   Wiki hii tutaongelea menu mbalimbali ambazo waweza kuzila/ kuzipata mida ya mchana, iwe upo mgahawani, hotelini, ofisini, nyumbani au penginepo ambapo msosi unapatikana.
    Waweza share nasi ni menu gani unapata nyakati za mchana na pia utueleze unaipatia wapi na hata inakucost pesa ngapi. 
 Tupo pande za Samaki Samaki iliyopo katikati ya jiji la Dar iliyo salama pale kwenye jengo jipya. karibu uwatembelee.


   Chipsi zao ni zile zipo katika style hiyo, aina ya mkato wa vipande vikubwa. Halafu pembeni ni vipande vya samaki vikisindikizwa na mchicha na vikorombwezo vya pilipili, mayonnaise, tomato sauce na ndimu.
      Ukifika ulizia Bruce lee fish. Naamini yapatikana katika maeneo yote ya Samaki samaki namaanisha mjini, survey na Mbezi.

Friday, May 24

Ijumaa ndo hii

    Leo hatuongei sana, tunashare nanyi supu ya leo ambayo ni ya ng'ombe...... Karibu!!

     Tunawatakia mapumziko mema ya wikiendi hii Rafiqs!!

Thursday, May 23

Kifungua kinywa -Alhamisi a.k.a New Furahi dei

   Wakati tunaendelea kunako mwisho wa wiki a.k.a weekend, tunabadili muelekeo wa menu ya asubuhi a.k.a kifungua kinywa. Leo tumetoka kwenye chai, tumesogea upande wa supu.
    Supu ni mlo ambao waweza nyweka muda wowote, ukianzia na asubuhi kama kifungua kinywa, mchana katika style ya mchemsho, jioni kupasha tumbo joto kwa wale ambao hawakula chochote siku nzima, na hata kwa wale ambao hunywa kabla ya mambo yetu yaleee, na usiku pengine tukitaka kukata yalee mambo yetu, au tunapohisi hatutaki na hatuna hamu ya kula mlo mwingine, basi supu huwa suluhisho.
   Kingine supu pia hutumika sana pale tunapougua maana ni rahisi kumeza, ukiondoa uji. Hivyo wengi hupendelea kuwapikia wale wanaowauguza. Supu hutumika kama kianzio mlo kwa wale ambao wanapata ile full mlo, yaani kuanzia starter, main course na desert. Kwasasa kwenye mashughuli mengi mathalani maharusi, imekua kama ni desturi kuanza na supu au mtori, wengine wanaanza na cold desert kabla ya mlo wenyewe a.k.a ubwabwa wa harusi.
    Tujuze, huwa unakunywa supu nyakati gani? na unapendelea supu ya aina gani?? mmh je, ya kuku, samaki, ng'ombe? mbuzi au mbogamboga, hizo ni baadhi tu ya aina za supu tulizotaja, ila Rafiq tujuze ladha uipendayo.


     Hapo juu ni supu ya kuku wa kienyeji ambayo ilikutwa pande za Kigoma pajulikanapo kama land of butter and cream.
    Leo ni Alhamisi a.k.a Ijumaa mpya..... furahieni siku hii na tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuamsha salama. Siku njema tunawatakia!! 

Wednesday, May 22

Jumatano tunafungua kinywa ajeee??

  Kwa wale tunaofungua kinywa na mlo wa chai ya rangi au hata ya maziwa yenye kutumia majani ya rangi, siku hizi tuna aina nyingi za majani ya chai ya kutumia tunywapo chai zetu. 
   Majani ya chai mengi huongezewa ladha au hutengenezwa na vyakula vingine ili kuleta ladha tofauti katika unywaji wake, na pia kwa wale ambao pengine hawataki kunywa chai ya aina moja basi hupata nafasi ya kubadili ladha ya chai vile wapendavyo.
   Pia kuna chai zinazotengenezwa maalumu kwaajili ya wale wanaopenda kumaintain miili yao, yaani walio kwenye diet ambapo chai zao huitwa slim tea kama tupo sahihi.
   Je, wewe unapenda chai iwe na ladha gani iwapo wanywa chai ya rangi au ya maziwa itumiayo majani ya chai yawe na ladha au bila ladha?
   Moja ya aina ya majani ya chai, yenye ladha ya tunda la peach ikiwa kwenye pakiti


   Ikiwa ndani ya kikombe tayari kwa kusidikiza mlo mzima wa asubuhi ya leo ambao ni kitumbua kimoja, andazi moja na soseji moja. 


     Karibu kutujuza upendvyo wewe?

Tuesday, May 21

Kifungua kinywa

   Leo tumekaa kimaswali maswali zaidi... 
  La kwanza, Jumanne ya leo umefungua kinywa wapi??? umekula ukiwa nyumbani? kitaani?eneo la kazi? mgahawani? njiani? bar?au wapi?
  Swali la pili ntakuuliza, ni je, umefungua kinywa aje??? tumekula kitumbua kama mimi? maandazi? mikate? mihogo? viazi vitamu? sandwich? supu? soseji? juisi? chapati? kiporo cha jana? au? mmmh tuambizane
  Swali la tatu je, ulikua unafungua kinywa na nani? familia? wafanyakazi wenzio? wafanyabiashara wenzio? wana wa kitaa? washkaji? Rafiqs? maadui katika kuleta amani? Mashostito? au peke yakooo?? tujuze!!


   Kifungua kiinywa changu asubuhi ya leo kilikua hivyo hapo juu. Chai ya rangi, vitumbua viwili na soseji moja, niliipata nikiwa eneo la kazi, pamoja na Rafiqs na wafanyakazi wenzangu.
   Anwani ni menutimes@gmail.com ndo tunapopatikana.

Monday, May 20

Kutoka kwa Rafiq Jumatatu hii

   Mmoja wa Rafiq alikwenda pande za State kikazi lakini pia akaongeza siku za kuzunguka kidogo kusafisha macho. Kutokana na urafiq tuliokua nao, alitukumbuka mara kwa mara alipokua anapata menu pande hizi na hii ni moja ya ushuhuda w amenu aliyopata.
   Kuna kuku na viazi kwa chini, pembeni kuna salad ikisindikizwa na sauce pamoja na kipande cha ndimu. 

 
   Hakika rafiq aliinjoy menu za huko. Uzuri alipotua tu akatuarifu kuwa anaanza mazoezi fasta ili kurejesha mwili baada ya kujiachia pande hizo.
  Welcome back Mjinja!!

Friday, May 17

Milk shake

   Kuna sehemu mbalimbali ambazo wanatengeneza na kuuza milk shake ambapo unapata za ladha tofauti tofauti. Je, we unapenda ya ladha gani na huwa waipata wapi ya kwako uipendayo zaidi?

    
Tunawatakia wikiendi njema yenye amani, usalama na upendo kwenu, familia zenu na marafiki zenu. Tunawapenda sana!!


Kutoka kwa Rafiq wa U.S.A

   Tunaangalia milo ya Rafiqs waliopo pande za United State of America, a.k.a kwa Obama. Waneshare nasi menu mbili ambazo zinafanana flani, angalia vyema


  Hii ya chini wamesema kwenye sahani ni food tilapia, spinach, pico de gallo with potatoes and broccoli.

   Yaonekana very delicious...... yaani menu imesimama mno!!

Thursday, May 16

Mlo Kamili

   Kutoka kwa Rafiq aliyeweza pata mlo kamili siku ya leo, anashare nasi menu aliyoipata pande za kitaani alipokua anapata lunch yake. Waweza pata na kuiinjoy menu hiyo popote upendapo iwe ni kwa muda wa mchana au usiku.

 
    Yaonekana tamu!!!

Wednesday, May 15

Chapati maji na rosti

   Jana tulifundishana namna ya kupika chapati maji na nina uhakika sote tumeelewa vyema, na sasa twaweza kuipika fasta kupita maelekezo.
   Nachopendea menu hii ni kwamba hainichukui muda kuipika afu ni tamu pia. Nashare nawe mimi niliisindikiza na mboga gani.


   Ni rosti ya mbuzi, yenye tui la nazi na vikorombwezo vingine. Ntaja tena kuwajuza kupika rosti ya mbuzi, ila jua tu sio tofauti sana na ya ng'ombe au kuku.
   Karibu kushare nasi ulisindikizia chapati maji yako na mboga gani baada ya kuipika. Tutumie huku menutimes@gmail.com

Ubunifu mgahawani - Jackies

  Kila moja wetu ana mapenzi na namna mlo wake utengenezwe, naongelea kwamba unakua na upishi wako mwenyewe ambao unajua kwamba utaufurahia na kuufaidi wakati unakula mlo wako.
   Tatizo linakuja pale umefika mgahawani na wao wana aina yao ya upishi, sisemi kwamba ni mbaya laaa, bali sio ule upishi wako unaoutaka wewe haswaa. 
   Baadhi yetu tunaona kwanini tusisemezane na mpishi, yaani tukamjuza namna ya kupika upishi wetu ili yeye apate kuuza na sisi tupate kuinjoy hiyo menu ambayo tunaagiza ikiwa na maelekezo ya namna ya upishi.
   Tulienda Jackies bar ya pale Oysterbay, niko mimi na Rafiq aitwa Abdallah Gunda, ambao tunapenda pilipili nyingi kwenye kila milo tunayokula tukiwa kwa ofisi. Sasa pale wana kuku foil, ambayo wana namna yao ya kupika, ila haina pilipili nyingi na mengineyo. Tukasemezana na mpishi, akafanya majaribio, akafaulu na toka siku hiyo tukipiga simu, twaagiza kuku foil Abdalah special.

  
   Kama inavyoonekana hapo juu fresh from foil. Unakua unaisindikizia na ndizi, ugali, wali, chipsi au hata hivyo hivyo inafaa tu. Sasa kama sio mpenzi wa pilipili waweza agizia huku ukiwataadharisha mapema kwamba wasiweke pilipili nyingi, na kama wataka kuijaribu yenye pilipili hakikisha maji ya kunywa yapo pembeni iwapo pilipili ikawa imekolea sana.
  Ni hayo tu toka kwetu wana Menu Time!!

Tuesday, May 14

Chakula cha usiku cha nyumbani.

   Kutoka kwa mwanafamilia, partner, mdau na Rafiq wa Menu Time, ameshare nasi menu aliyoipata jana usiku akiwa nyumbani kwake.
   Anasema aliipika mwenyewe na huyu ni bwana Tyik
 
   Kuna wali mweupe pamoja na rosti ya vipande vya kuku vilivyoungwa na tui la nazi. Pembeni alishushia na maji ya matunda ya machungwa, maana msimu si ndo huu!!
  Karibuni!!

Upishi wa chapati maji a.k.a pancakes


  Leo tunafundishana upishi wa chapati maji a.k.a pancakes. Kila mmoja wetu ana namna yake ya kupika kutokana na kupenda chapati maji hiyo itokee na ladha gani. Leo Menu Time katika upishi huu tunatumia viungo tofauti kidogo katika kuongeza ladha kwa mlaji. Karibuni!!

Mahitaji:
  • Unga wa ngano - kikombe kimoja na nusu
  • Maziwa kikombe kimoja
  • Yai moja
  • Blue band kiasi (kwa ajili ya kukaangia chapati maji zako)
  • Chumvi- nusu kijiko cha chai
  • Sukari - kijiko kimoja cha chai
  • Asali kijiko kimoja cha chai
  • Unga wa Cocoa kijiko kimoja cha chai
  • Kitunguu maji nusu
Hatua:
  • Chukua chombo kikubwa cha kutosha kuchanganya viungo vyako. Weka unga, pamoja na maziwa na yai kisha koroga kwa pamoja. Hakikisha vimekorogeka vyema, kisha katakata vitunguu maji katika vipande vidogo vidogo sana, kisha changanya na mchanganyiko wako. Ongeza chumvi, sukari, unga wa cocoa pamoja na asali kisha koroga mchanganyiko wako kwa kutumia mwiko wa mbao hadi mchanganyiko wako uwe umechanganyika vyema na hauna mabongebonge.
  • Mchanganyiko utaonekana kama hapo chini kwenye picha
  •  Weka kikaangio kwenye moto, kisha acha kipate joto na ongeza kijipande cha blue band kidogo ili kuzuia chapati maji isigande kwenye kikaangio
  • Weka mchanganyiko wa chapati maji kwa kupima, vijiko viwili vya kupakilia, kisha tandaza kwenye kikaangio ili kutengeneza umbo la duara
  • Acha chapati maji ipate kuiva vyema kwa kuiacha ikauke upande wa juu kabla ya kuigeuza, kama inavyoonekana kwenye picha
 
  • Geuza chapati maji yako na kuiacha ipate kuiva vyema upande wa pili, kuwa makini ili kuzuia chapati maji kuungua lakini hakikisha imeiva vyema. Utakapoigeuza, upande wa mwanzo utaonekana kama ilivyo kwenye picha hapo chini
  • Baada ya kuhakikisha upande wa chini/ pili nao umeiva, epua chapati maji yako tayari kwa kuliwa na walaji wako

Chapati maji yaweza kuliwa na kitu chochote iwe ni chai, maziwa, mboga yeyote, soda au hata hivyo hivyo, ikitegemea na umejiandaaje na mlo wako.
   Kuna wanaokula kama kifungua kinywa, kuna wale wa cha mchana au usiku na wengine kama bites, inategemea na muda gani ungependa kupata mlo wako wa chapati maji

   Mpaka hapo tunakua tumefika mwisho wa mapishi ya chapati maji a.k.a pancakes yenye maziwa n.k.
   Kushare nasi namna ya kupika menu yoyote, wasiliana nasi kupitia barua pepe menutimes@gmail.com

Monday, May 13

Viazi mviringo na rosti

   Kama kawaida ya mwisho wa wiki, kuna karatiba ka kutembelea ndugu, jamaa na marafiq, wikiendi hii, tulikatiza kwa mama Lulu na kuamua kulibariki jiko lake, kwa kuandaa viazi mviringo vikiwa na maganda yake pamoja na rosti ya mbuzi.
   Upishi wake ni rahisi sana, kwani wahitaji kuviosha viazi hadi viwe safi kabisa. Chukua sufuria safi yenye maji kidogo, kisha weka vipande vya viazi, chukua kitunguu maji, katakata kitunguu maji na weka pamoja na viazi, ongeza chumvi na weka jikoni vipate kuchemka kidogo, kama dakika 5 hivi.
   Hakikisha havichemki kabisa kwani vitapondeka, bali vinapata kulainika kidogo, kwani viazi hivi vitakaangwa kwenye mafuta. Epua viazi vyako, chuja kuondoa maji kisha weka kikaangio kwenye jiko, ongeza mafuta kisha acha yachemke na kaanga viazi vyako vikiwa na maganda yake.
   Muonekano unakua kama hivyo hapo kwenye picha

     Jaribisha upishi huu, unakua huchoki kula viazi vya mpiko mmoja, bali wabadilisha style. Ukishapika tutumie picha tuone vimetokelezeaje. Pembeni ni kikorombwezo cha kusindikizia menu hiyo.

Lunch ya Leo a.k.a Cha mchana!!

   Tulipokua kitaani leo, hii ndio menu tuliyokutana nayo. Kuna wali mweupe, ndizi zilizoungwa pamoja na nyama, pembeni kuna mboga za majani kukamilisha lishe bora ya mchana. Kishushio ilikua ni maji baridi pamoja na tunda la chungwa

 
           Menu yote hiyo ilikost jumla ya shilingi elfu tatu tu za kitanzania,

Sunday, May 12

Siku ya kina Mama Duniani!!

   Siku ya leo ni siku muhimu iliyotengwa kwa ajili ya kina mama wote duniani. Na kutoka timu ya Menu Time tunawatakia kina mama wote kila la kheri katika kulea watoto wote, pamoja na kuwapa pole kwa majukumu mazito sana ya ulezi.
   Hatuna cha kuwapa zaidi ya neno Shukrani !!!
   Asanteni sana Mama zetu woote!!

Thursday, May 2

Kitaani na chipsi

  Moja ya menu inayopendwa sana naRafiqs wengi ni chipsi a.k.a kiepe. Sasa utaamua wataka kiepe iliyochanganywa na mayai a.k.a zege, au kavu ikisindikizwa na soseji, mishkaki au kuku au kingine kama maini, salad n.k
   Tujuze wewe unapenda chipsi za wapi?, maana wengi wanasema zile ze kitaani ni tamu zaidi kuliko za nyumbani.
   Katika pita pita zetu pande za Kinondoni huku Dar iliyo salama, tukakutana na zege yaani chipsi iliyochanganywa na mayai likisindikizwa na salad.... karibuni!!

Supu ya mbuzi shughulini

   Jana kuna Rafiqs waliamua kuchinja mbuzi na kunywa supu pamoja na kula nyama. Sasa kukamilisha hilo lote, tukaalikwa marafiq katika mnuso huo, na kwasababu hatuna tabia ya kusema sana, ushahidi wa yalojiri ni huo hapo chini. Twashare nanyi picha ya supu ya mbuzi pamoja na ndizi za kuchemsha.
   Kwanza kuna sufuria la supu, kisha kuna kibakuli cha supu ya memba wa Menu Time aliyoifaidi jana. Asante sana Rafiq muendelee kutualika Menu Time.

Wednesday, May 1

Upishi wa viazi vyenye maganda

   Kuna namna tofauti ya kupika viazi yaani vile vya kukaanga. Hii ni pale unapoamua kupika pamoja na maganda yake.
   Cha kuzingatia ni kuhakikisha unaviosha vyema viazi vyako kabla ya kuvipika, hakikisha mchanga wote umetoka na viazi ni visafi mno.
    Kisha kata vipande vya ukubwa kiasi na viweke kwenye sufuria yenya maji safi. Katakata vitunguu, kisha ongeza chumvi na pilipili manga kidogo kisha weka kwenye jiko na viache vipate kuchemka kidogo sana, vilainike kwa mbali.
   Epua viazi vyako na uchuje maji, kisha weka kikaangio kwenye jiko, weka mafuta na yakipata moto, weka viazi viweze kukaangika vyema. (usimenye maganda).
    Viazi vikishaiva na kugeuka rangi, epua tayari kwa kuliwa, vipange kwenye chombo safi kama sinia kisha kwaruzia jibini kwa juu na karibisha rafiqs mlo wa usiku.
    Ndizi ni aina ya mzuzu ambapo unazimenya kisha wavikata katikati na kuvikaanga vyema mpaka ziive. Epua tayari kwa kuliwa.
    Waweza kula na mboga yeyote uipendayo!!!


Tambi a.k.a Macaroni

   Kutoka kwa memba wa Menu Time aishiye Marekani, ameshare nasi menu aliyoipata pande za West Virginia. Chakula chaitwa spaghetti n chicken!
   Kilikua ni chakula cha usiku toka pande hizo!!