Wednesday, July 2

Mtori wa mgonjwa

Tukiwa tunalea wagonjwa tumeletewa mtori na mama wa mama Menutime, yaani bibi Menutime. Mtori ni moja ya chakula ambayo ni rahisi kupika na pia kuliwa na mgonjwa maana anafanya kumeza tu ambapo hahitaji kutafuna sana.
Basi leo tumeletewa mtori na bibi na huu ni kama ule wa nyumbani Rombo, maana sie si wachagga ivo tukarejea nyumbani.

                            
Kwenye makala zetu huko nyuma tumewajuza namna ya kupika mtori, karibu ujifunze usipate shida kumlea mgonjwa wako nyumbani au hata hospitalini iwapo utapaswa kupeleka menu.
  Twawapenda sana sana, na twamtakia mgonjwa wetu apone haraka.

No comments:

Post a Comment