Wednesday, May 15

Ubunifu mgahawani - Jackies

  Kila moja wetu ana mapenzi na namna mlo wake utengenezwe, naongelea kwamba unakua na upishi wako mwenyewe ambao unajua kwamba utaufurahia na kuufaidi wakati unakula mlo wako.
   Tatizo linakuja pale umefika mgahawani na wao wana aina yao ya upishi, sisemi kwamba ni mbaya laaa, bali sio ule upishi wako unaoutaka wewe haswaa. 
   Baadhi yetu tunaona kwanini tusisemezane na mpishi, yaani tukamjuza namna ya kupika upishi wetu ili yeye apate kuuza na sisi tupate kuinjoy hiyo menu ambayo tunaagiza ikiwa na maelekezo ya namna ya upishi.
   Tulienda Jackies bar ya pale Oysterbay, niko mimi na Rafiq aitwa Abdallah Gunda, ambao tunapenda pilipili nyingi kwenye kila milo tunayokula tukiwa kwa ofisi. Sasa pale wana kuku foil, ambayo wana namna yao ya kupika, ila haina pilipili nyingi na mengineyo. Tukasemezana na mpishi, akafanya majaribio, akafaulu na toka siku hiyo tukipiga simu, twaagiza kuku foil Abdalah special.

  
   Kama inavyoonekana hapo juu fresh from foil. Unakua unaisindikizia na ndizi, ugali, wali, chipsi au hata hivyo hivyo inafaa tu. Sasa kama sio mpenzi wa pilipili waweza agizia huku ukiwataadharisha mapema kwamba wasiweke pilipili nyingi, na kama wataka kuijaribu yenye pilipili hakikisha maji ya kunywa yapo pembeni iwapo pilipili ikawa imekolea sana.
  Ni hayo tu toka kwetu wana Menu Time!!

No comments:

Post a Comment