Thursday, April 11

Toto day ya tarehe 23.03.2013

   Tunazidi kusonga mbele kwa picha ... karibuni!!
Kulikua na face painting a.k.a kuchora nyuso, hata miss LJM alipata kuchorwa uso wake

Kids entertainment world, walitimiza promise yao na tulijump kwenye castle a.k.a mahekalu kwa raha zetu.

  Halafu tukahamia kwenye muziki, tukaimba, tukarukaruka na kucheza muziki kutoka kwa Dj Rico wa Mbalamwezi Beach club

  Batman ndo alikua msimamizi mkuu wa michezo ya watoto, naye ni mmoja au timu ya Kids entertainment world, hakika alisherehesha vyema
    
 Hawaa wa Bayumi alikuwepo na wanae katika kufanikisha shughuli hii, asante sana Mama watoto.

  Kwa wale waliopenda kucheza na maji, mipira ya kuogelea ilikuwepo na ulinzi maalumu, ambapo watoto waliogolea wakidhani samaki. ilikua furaha tu

  Tulichora michoro tofautitofauti katika sura zetu na uzuri, michoro ilichorwa kwa ustadi na dada kutoka Kids entertainment world, na uzuri hizi rangi hazina madhara na ukiosha na maji tu hata bila sabuni inatoka fasta

Vikaragosi watu walikuwepo kuongezea utamu wa shughuli ambapo walicheza vyema na watoto. Ilikua raha kuwa na vikaragosi karibu, kuwashika na kupiga nao picha.
  Bado kuna mengi ya kukuhadithia ila tutamalizia siku zijazo..... kwa leo kama vile tuishie hapa kwanza...

No comments:

Post a Comment