Wednesday, March 13

Wadhamini wa Toto day ya tarehe 23.03.2013

   Leo tunawaangalia wanaotuwezesha Menu Time na K.A.B.L.E katika kuifanikisha ndoto ya watoto wa Malaika orphanage Foundation wa Kinondoni kuwa kweli. Ndoto yao au ombi lao lilikua ni kwenda ufukweni wakati wa Pasaka, ila kutokana na mengi yatakuwa yanaendelea wakati huo, tukaona ni vyema kufanya kabla ya hapo, ili kutoa nafasi kwa familia kuenjoy pamoja kama walivyyopanga katika kusherekea Pasaka.
   Tunasema Asanteni sana wadhamini wetu, maana nyie ndio mnaofanikisha shughuli hii ya watoto, na kwa upendo wenu mlionao kwa watoto mmejitolea kwa kile mlichonacho, na kwa hilo kwa niaba ya watoto na uongozi wa Malaika Orphanage Foundation tunasema Asanteni sana sana!!
   Tunao Mbalamwezi Beach Club - Club ya ufukweni ambapo utapata mambo mengi ya kupendeza iwapo wataka kupata upepo mwanana wa baharini. Kuna vinywaji vya aina zote, vyakula tele, huduma nzuri, muziki murua na mandhari ya kuvutia. Mbalamwezi ndo eneo ambalo Toto day itafanyika.
   
    Tunao Kids Word Entertainment - hii kampuni inahusika na mambo yote ya jumping castle, kuchora sura za watoto, michezo ya watoto, vikaragosi n.k, watakuwepo siku hiyo katika kuhakikisha watoto wanapata raha tunayoitarajia.
                              
 

   Tunao Airtel Tanzania, Mtandao wa washkaji ambao watahakikisha mawasiliano toka utayarishaji wa Toto day, kufanyika kwa Toto day na baada  ya Toto day bado washkaji tunawasiliana. Pia watasaidia kufikisha ujumbe kuhusu Toto day kuweza wafikia washkaji wengi ili waweze kuja na wanao na kuendeleza ushkaji.
    Wengine wadhamini wetu ni Prime advertising, The Mboni show, Achick Investment na The Esquire Room ambao watakua na jukumu la kuwanyoa watoto nywele kabla ya kuja kufurajia siku hii


Asanteni sana nyote kwa kuwa pamoja nasi katika kuhakikisha Toto day itakuwa nzuri na sababu ya mabadiliko katika maisha ya watoto wa Malaika Orphanage Foundation

No comments:

Post a Comment