Tuesday, March 26

Nakuonjesha yalojiri Jumamosi iliyopita pale Mbalamwezi kwenye Toto Day!!

   Tunamshukuru Mungu sana kwa kutuwezesha kuamka salama, kuweza kuhudhuria siku ya Toto day tukiwa wazima, kwa kutukutanisha na marafiq wengi sana Jumamosi ile iliyopita pale Mbalamwezi Beach Club!! Ukweli ni kwamba siku ilikua nzuri sana na tulipata na baraka ya mvua iliyopita kidogo kisha michezo iliendelea kama kawaida.
    Watoto walicheza, walirukaruka, waliimba, walidance, walikula, walikunywa, waliogelea na kadhalika kiujumla tunasema waliinjoi siku yao malumu wakiwa na wenzao kutoka Malaika Orphanage Foundation. Asante sana wadhamini wetu Airtel, Mbalamwezi Beach Club, Kids world Entertainment, Sayona, The Mboni show, Achick investment pamoja na The Esquer spur kwa udhamini, upendo na kuwa pamoja na sisi siku hiyo. Asanteni sana!!
    Tutakuja waonesha yaliyojiri kwenye picha nyingi, ila kwa kukuonjesha tuliweza kubandika na kuweka alama za mikono kwenye kitambaa ikiwa ni ishara ya kumbukumbu yetu pamoja. 
 
 `

   Lulu John M a.k.a LJM wa Menu Time akiweka alama ya kiganja cha mkono kama kumbukummbu ya uwepo wake siku ya Toto day.
   Endelea kutembelea www.menutime.blogspot.com kujua zaidi yaliyojiri!!

No comments:

Post a Comment