Tuesday, July 3

Menu Time & T-Bonaz

Menu Time na T-Bonaz ni marafiki katika mambo meeengi.. na June 30 ya Safari Lager Nyama Choma Festival, walikuwa pamoja kuhakikisha swala zima la uchomaji wa nyama pamoja na upatikanaji wa salad a.k.a Kachumbari. Basi ulivokuwa ukifika kwenye Banda la T-Bonaz unajipatia nyama ya kuku na T-Bone.. lakini Pia ulikuwa Huru kuchagua Kachumbari saaafi iliyoandaliwa na MT Team..
 T-Bones zilichomwa mpaka zikaelewa somo, wateja wa Banda la T-Bonaz walipata wasaa wa kujipatia Ndizi Choma Pia...
 Nyama hainogi bila Kachumbari bhana.. kwa kuelewa hilo Metu Time walitokezea na wazo zuri la kuwaandalia wateja wetu salad a.k.a kachumbari za aina mbalimbali...
Kulikuwepo salad ya Prawns, salad ya mboga mboga bila kusahau salad yetu ya kawaida kabisa, salad ya nyanya, kitunguu na ndimu...



 Menu Time na T-Bonaz walifanya vizuri sana wasiliana nasi kwa ushauri juu ya mambo ya salad na T-Bones... karibu Menu Time..

No comments:

Post a Comment