Tuesday, May 29

Mahindi ya Kuchoma na ya Kuchemsha.

   Katika pita pita zetu kitaani leo tukawakuta wana wa Jiji wakiwa wanajiongezea kipato kwa kuchemsha, kuchoma na kisha kuyauza yakiiva.
 Hapo sasa unachukua hindi lako unalipakaa pilipili na ndimu, ukiangalia picha hiyo hapo juu hicho kibakuli chenye chumvi nyekundu ndo pilipili hiyo.
Basi unajipatia kipande chako cha shilingi 100,200 au 300 mfuko wako utaamua.
  Kwa Dar es salaam mahindi yanauzwa sana kipindi mvua ikinyesha. Bado sijajua sababu ni nini kama unaijua waweza changia hapo chini. Karibu.

No comments:

Post a Comment