Ni sehemu tulivu, unaamua kukaa chini ya mjengo au chini ya mti, unatoa oda yako na wanakutengenezea fasta kuliko maelezo.
Wana menyu mbalimbali, naongelea ndizi za kupikwa na nyama (ni tamu sijapata kula Dar), wanachoma kuku, mbuzi, ng'ombe, ndizi, kuna chipsi, maini, chapati na mengine mengi utayaona ukifika kwa kweli.
Nakuonesha kiduchuuuu tuuu, menyu yao niliyoikuta siku hiyo:
Kuku haoo wako tayari, dada yangu anawaita vyuku....
Mishkaki na mguu wa naniiiii kwa mbali.....
Mmmhh kwa karibu vyuku haoo....
Kuna samaki pia wakukaanga na wa mchuzi wapo pia....
Kuku akiwa tayari kwa kuliwa,kakatwakatwa vipande kadhaa na kasalad kwa mbaaali....
MMMMh salad yao ni fresh aseeeee.....
Fanya juu chini upate pitia hapo nawe uonje mahanjumati. Menu Time ikisema hapo ni pema na menyu yake ni tamu amini ni patamu. Pitia uhakikishe hilo.
No comments:
Post a Comment